UNESCO yapitisha mwongozo wa kihistoria kuhusu jukumu mtambuka la elimu katika kukuza amani
Mnamo tarehe 20 Novemba 2023, Nchi 194 Wanachama wa UNESCO zilipitisha Pendekezo la Elimu kwa Amani, Haki za Binadamu na Maendeleo Endelevu katika Mkutano Mkuu wa UNESCO. Hiki ndicho chombo pekee cha kimataifa cha kuweka viwango ambacho kinaweka bayana jinsi elimu inapaswa kutumika kuleta amani ya kudumu na kukuza maendeleo ya binadamu kupitia kanuni 14 elekezi.